Posts

Showing posts from November, 2019

UTACHEKA: John Cena kaambiwa aimbie ‘John Cena’ ya Sho Madjozi

Image
Ni  Headlines  za mcheza mieleka ambae kwasasa vichwa vya habari vimerudi huko Marekani baada ya msanii wa  Afrika Kusini  aitwae  Sho Madjozi  kutumia jina lake katika wimbo wake uitwao  John Cena. Sasa utacheka pale ambapo  John Cena  alipofika katika kipindi cha  Strahan Sara and Keke  huko Marekani na kuambiwa aimbie wimbo huo wa msanii wa Afrika Kusini.

Heshima aliyopewa Nipsey Hussle na waandaji tuzo za Grammy’s 2019

Image
NI Headlines za waandaji wa tuzo za  Grammy’s  ambapo wametoa heshima kwa The Late Rapper Nipsey Hussle kwa kuweka suti aliyowahi kuivaa rapper huyo katika tuzo zilizopita. Waandaji hao wameiweka suti hiyo katika jumba lao la Makumbusho huko nchini Marekani ikiwa katika kumuenzi rapper huyo. Nipsey Hussle pia ametajwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo hizo kubwa za muziki za mwaka 2020 ikiwemo,  Best Rap/Sung Performance, Best Rap Performance na Best Rap Song.

Lulu alivyomjibu jamaa aliemtongoza mtandaoni

Image
Staa Elizabeth Michael Lulu, amemjibu mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Nasri Mchemwa ambaye alimtumia ujumbe wa kutaka kuwa naye kwenye mahusiano. Elizabeth Michael ✔ @OfficialLizyM Asante Baba https:// twitter.com/nasrimchemwa/s tatus/1197731729005527040  … nasri mchemwa mwampashi @NasriMchemwa Replying to @OfficialLizyM umeamkaje elizabeth michaelofficial lulu.mzima my love.nakusumbua sana sio mm bali nimoyo wangu unasababisha niteseke juu yako kuusu upendo ulio ulondani yangu.usinione http:// nakutania.ni   umaskini tu,nilionao ningejitoa kwa vyovyote ili uamini sio utani,nakupenda hadi basi 808 2:34 PM - Nov 23, 2019 Twitter Ads info and privacy Jamaa aliandika hivi -“ umeamkaje Elizabeth Michael Lulu, mzima my love nakusumbua sana ila sio mimi bali ni moyo wangu unasababisha niteseke juu yako kuhusu upendo ulio ndani yangu “  “Usinione nakutania ni umaskini tu,nilionao ningejitoa...

Pamoja na kupoteza Samatta ana wastani mzuri wa magoli Champions League

Image
Mtanzania Mbwana Samatta licha ya timu yake ya KRC Genk kupoteza kwa kufungwa magoli 4-1 dhidi ya RB Salzburg katika mchezo wao wa tano wa UEFA Champions League, Samatta anaendelea kujiweka sokoni kutokana na kuendelea kufunga. Katika mchezo wao wa tano akicheza na KRC Genk Champions League ambapo tayari wameshaondolewa, Samatta alifunga goli la kufutia machozi dakika ya 85 na hilo kuwa goli lake la tatu Champions League akicheza jumla ya michezo mitano, kitu ambacho kitamuweka pazuri katika dirisha la usajili la mwezi January kiasi cha kuweza kuonekana na timu mbalimbali.

Casto kamjibu Tunda “Wewe ni video vixen tu unakuja kuniambia nini, message za kuedit”

Mtangazaji wa  Clouds TV  kupitia kipindi cha Sizi kitaa  Casto Dickson  ambaye aliwahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na Mrembo  Tunda  amefunguka na kumjibu EX wake huyo ikiwa ni siku chache toka  Tunda  avujishe mtandaoni message ambazo Casto amekuwa akimtumia Whtsap. C asto amesema yale aliyoandika Tunda siyo kweli…. “Kwanza siyo kweli, Mimi ninachowaombea kama kuna hatua wamepiga baada ya kuongea hivyo Mungu awabariki, Mimi nafanya mambo yangu Niko Kwenye levels nyingne, Huwezi kunifanya Mimi kuwa Maarufu miaka kumi, Alafu unakuja kuniambia umenifanya Mimi kuwa maarufu wewe ni nani..? Wewe ni video Vixen tu unakuja kuniambia nini..? Message za kuedit “  –  Casto Dickson

Maamuzi ya mashabiki wa Malmo Sweden, baada ya kusikia Zlatan kanunua timu pinzani

Image
Mshambuliaji wa zamani wa timu za FC Barcelona, Inter Milan na LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic amekuwa gumzo mitandaoni kufuatia mapokeo ya uamuzi wake wa kununua asilimia 50 ya hisa za timu ya Hammarby inayoshiriki Ligi Kuu Sweden Kufuatia maamuzi hayo wakati huu Zlatan akiwa kamaliza mkataba wake na club ya LA Galaxy ya Marekani, mashabiki wa timu yake iliyomuibua utotoni nchini kwao Sweden club ya Malmo wameamua kuchoma moto sanamu yake iliyokuwa imejengwa nje ya uwanja wa Malmo kwa heshima na kumuenzi mchezaji huyo. Mashabiki hao wanamuona Zlatan ni kama msaliti kwenda kununua club pinzani, kwa Malmo iliyomubua na kumpa heshim na Malmo katika Ligi Kuu ya Sweden, hata hivyo timu ya Hammarby na LA Galaxy zote zilikuwa chini ya  umiliki wa kampuni ya AEG Sweden kabla ya Zlatan kunua hisa Hammarby

Mama wa Sharo Milionea kazungumza wasanii waliomtenga ‘Mimi Mlemavu’

Image
Mama mzazi wa marehemu  Sharo Milionea  amezungumza kuhusu kumbukumbu ya siku ya kifo cha mwanae kilichotokea November 26 miaka saba iliyopita ikiwa kila ifikiapo siku hiyo humfanyia kisomo huko nyumbani kwake Tanga, Mama Sharo amesema kipindi cha nyuma baadhi ya wasanii waliokuwa karibu na mwanae walikuwa wakishiriki naye tofauti na sasa. Mama Sharo amezungumza ikiwa ni siku ambayo baadhi ya wasanii wakiongozwa na  Irene Uwoya  walikwenda nyumbani kwake Tanga kumtembelea na kufanya kisomo kwaajili ya marehemu Sharo Milionea.

Rihanna alivyoibuka kwenye mechi ya Juventus dhidi ya Atletico Madrid

Image
Ni Headlines za mwimbaji wa kike kutokea nchini Marekani aitwae  Rihanna  ambae jana alifika uwanjani kushuhudia mchezo wa Juventus dhidi ya  Atletico Madrid Ambapo mpira ulimalizika ndani ya dakika 90 ulikwisha Juventus 1-0 Atletico,  Rihanna  alionekana uwanjani akiwa na pochi ya Louis Vuitton yenye thamani ya paundi   Elfu 2000  ambazo ni sawa na milioni 5 za kitanzania.  

Baada ya kulazwa kwa sita kwenye chumba cha ICU rapper French Montana atabasamu

Image
NI Headlines za rapper wa kike,  Megan Thee Stallion  kutokea nchini  Marekani  ambae amefika kwenye hospitali aliyokuwa akipewa matibabu rapper  French Montana  na kuwadhihirishia mashabiki hali yake inaendelea vizuri. Hapo awali iliripotiwa taarifa juu ya  French Montana  kufika katika moja ya hospitali kubwa nchini Marekani kupatiwa huduma ya matibabu ya maumivu aliyokuwa akiyasikia katika tumbo lake kisha kupelekea kulazwa kwa siku sita kwenye chumba cha ICU. Rapper huyo anatarajiwa siku ya Ijumaa Novemba 29 kuruhusiwa kwenye nyumbani endapo afya itakuwa imara, hapa chini nimekuwekea video ujionee msanii mwenzake alipofika hospitalini kumjulia hali

Navy Kenzo, Joh Makini Gnako kwenye Stage Moja na Burna Boy DSM

Image
Siku ya Ijumaa November 29, 2019 linatarajiwa kufanyika tamasha la muziki litakalo mdondosha mkali kutokea Nigeria  Burna Boy  ambaye atafika Tanzania kwa mara ya kwanza kwaajili ya kufanya show ambapo kwenye stage ataungana na wasanii wa muziki wa Bongo Fleva ambao ni  Joh Makini ,  Gnako  pamoja na kundi la  Navy Kenzo. Wasanii hao wa  Bongo Fleva  watakao panda kwenye stage moja na Burna Boy wamejigamba kuwa watamkalisha msanii huyo wa Naigeria kwenye tamasha hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Next door Arena Jijini Dar Es Es Salaam. “ Tunajisikia furaha kuwa miongoni mwa wasanii tutakao toa burudani pale, na hii itakuwa mara yetu ya pili kuperform same stage na Burna Boy maana kuna kipindi tuliperfom SA na sasa hivi tunamkaribisha hapa nyumbani, Tunamkaribisha kila mtu na kama unavyojua mahali walipo Navy Kenzo lazima moto uwake”   – Nahrea Mimi Binafsi najisikia kuheshimiwa lakini pia naona muziki wa Hip Ho...